WANANCHI WAILILIA SERIKALI KWA KUBOMOA MAKAZI YAO


Na Emmanuel Matinde, Kigoma

Wakazi wa Mitaa ya Rutimba na Kitenge Kata ya Machinjioni katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameangua kilio kufuatia serikali kuanza kubomoa nyumba zao zinazodaiwa kuwa ndani ya eneo la ukanda maalum wa uwekezaji KISEZ, baada ya kushindwa kuondoka wenyewe kwa hiari licha ya serikali kueleza imeshalipa fidia ya maeneo hayo tangu mwaka 2009.

Zaidi ya nyumba 300 zinakumbwa na kadhia hiyo huku wakazi hao wakiishutumu serikali ya mkoa wa Kigoma kwa hatua hiyo ambayo imewaacha bila makazi ya kuishi na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia katika suala hilo.

Aidha wakazi wa kata jirani ya Kagera, wanaonyesha kuguswa na yaliyowakuta ndugu zao wakihofu siku moja kutimia kwa ule usemi kwamba yaliyomkuta Boko na Mamba yatamkuta.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mkoa Kigoma Special Economic Zone, KISEZ, ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma anayesimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji Deogratius Sangu, amesema zoezi hilo linalenga kuweka mipaka ya eneo hilo.


Post a Comment

0 Comments