WAZIRI KAIRUKI AJIPANGA KUDHIBITI UTORO WA WALIMU NA WANAFUNZI

Na Mwandishi Wetu, Tanga
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko mbioni kuja na mwarobaini wa kukomosha utoro wa wanafunzi na walimu.

Haya yameelezwa jijini Tanga na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki Tar 16.01.2023 wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri kwenye kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika shule ya sekondari Tanga ufundi

Amesema tangu niingie katika wizara hiyo amekuwa akitafakari kuja na mkakati wa kudhibiti utoro wa walimu na wanafunzi.

“Nilikuwa nazungumza na Naibu Katibu Mkuu (Dk Chareles Msonde), tangu nimeingia miezi hii mitatu najipanga kuona tufanyeje kukomesha utoro.”

“Naamini muda si mrefu tutaweza kuja na suluhisho la suala hilo na mtakuja kuona muda si mrefu.”

Post a Comment

0 Comments