KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI NCHINI YASHAURIWA KUJIANDAA KIBIASHARA


Na Emmanuel Matinde, Kigoma

Wakati serikali ikitarajia kuanza ujenzi wa meli mbili zitakazofanya kazi katika Ziwa Tanganyika, Kampuni ya Huduma za Meli nchini MSCL, imeishauriwa kujiandaa vizuri kibiashara na kuwa wabunifu ili kutumia fursa zilizopo kwa kuweza kushindana kibiashara na meli za nchi jirani.

Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 24 kwa ajili ya kujenga Meli mbili mpya za migizo na abiria katika Ziwa Tanganyika, na Shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kujenga cherezo kitakachotumika kwa ujenzi wa meli hizo, huku nchi jirani ya Congo DRC ikijenga Meli nane katika muda mfupi ujao hali inayoashiria kuwepo kwa ushindani wa biashara ya usafirishaji siku zijazo.

Kutokana na hali hiyo Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC kupitia kwa Mwenyekiti wake wa Bodi, Kapteni Musa Hamza Mandia, akizungumza baada ya kutembelea Meli za Kampuni ya Huduma za Meli na kukagua ukarabati wa Meli ya mafuta ya MT SANGARA, katika Bandari ya Kigoma amesema.

Kapteni Mandia amesema Meli zitakazojengwa ni kubwa hivyo  ni lazima wahakikishe wanapata mzigo wa kuweza kujaza meli hizo lakini sambamba na hilo wahakikishe wanakuwa na watu wenye sifa za kuendesha meli hizo.

Kaimu Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini MSCL tawi la Kigoma, Allen Butembero amesema ujenzi wa meli hizo unatarajia kuanza ndani ya miezi mitatu ijayo huku akizungumzia sehemu ya maandalizi ya kibiashara.

Post a Comment

0 Comments