TAMISEMI YAWATAKA VIONGOZI KUDHIBITINI UVUJISHWAJI WA SIRI NA NYARAKA ZA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde amewataka Makatibu Tawala, Wakuu wa Idara katika Mikoa na  Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti  uvujishaji wa  siri na nyaraka za Serikali kwakuwa suala hilo bado ni changamoto.

Mhe. Silinde amesema hayo Februari 23, 2023 Jijini  Dodoma  wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali.

 Amesema, hali ya utunzaji wa nyaraka hauzingatiwi kama inavyotakiwa katika maeneo wanayosimamia.

"Bado kuna baadhi ya watumishi mnaowasimamia  wanabeba majalada ya siri yakiwa hayajafunika, wengine wanakwenda na nyaraka za Serikali nyumbani"

Amefafanua kuwa hali hiyo husababisha usalama wa nyaraka za Serikali kutozingatiwa na hivyo kuhatarisha ustawi wa Taifa.

Mhe. Silinde  amewataka maafisa hao kudhibiti suala hilo na hasa zama hizi za utandawazi kuwa mstari wa mbele kutunza siri za Serikali.

“mmeaminiwa nendeni mkadhibiti uvujishwaji wa siri za Serikali katika zama hizi za utandawazi muwe mstari wa mbele katika kuzitunza,”amesisitiza 

Ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kuongeza uadilifu katika utumishi wa umma na hasa kwa watumishi wa Mikoa na Halmashauri  mnaowaongoza na kuwasimamia.

Ameongezea kuhusu ukusanyaji mapato, Mhe. Silinde amewataka watendaji hao kuhakikisha wanaibua vyanzo vipya na kuendelea kupanga rasilimaliwatu  katika ukusanyaji wa mapato na wakati mwingine kushauri namna nzuri ya kupata rasilimali watu ili kusaidia kukusanya mapato katika mazingira yenye uhaba wa watumishi.

Akizungumzia kuhusu taratibu za uendeshaji wa mashauri ya nidhamu kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, amesema baadhi yamekuwa hayahitimishwi kwa wakati au watumishi kutokupewa fursa ya kujitetea kwa mujibu wa  kanuni na hivyo kutowatendea haki.

Amesema Serikali ilianzisha utaratibu wa kufuatwa katika kushughulikia masuala ya nidhamu kwa watumishi wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“ Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi katika kushughulikia masuala ya nidhamu za watumishi.

Post a Comment

0 Comments