THPS KUIBUA ASILIMIA 28 YA WATU WENYE VVU KIGOMA


Na Adela Madyane, Kigoma

Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) kupitia mradi wa Afya Hatua unaofadhiliwa na shirika la Kimarekani la Centres for Diseases Control (CDC) imefanikiwa kuibua watu 988 katika kipindi cha robo ya Oktoba -Disemba 2022, sawa na  asilimia 28 ya lengo la mwaka kuwafikia watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoani Kigoma


Hayo yamebainishwa na Frederick Ndossi mkurugenzi wa Tiba na Matunzo wa mradi huo kwa mkuu wa mkoa wakati wa ziara ya kikazi ya mkurugenzi mkazi wa CDC yaliyofanyika katika maeneo ya mradi ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Kasulu pamoja na kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.


“Tunahakikisha wote waliobainika wanapata hamasa ya kutumia dawa ipasavyo kwa kuwaunganisha na wateja marafiki ili kuwatia hamasa na wajue jambo hilo sio lao peke yao” Amesema Ndossi


Kwa upande wa kuzuia virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto amesema watoto hupimwa afya zao mara tu wanapozaliwa na kuanza tiba kwa wale wanaokutwa na maamubizi na ambao hawakutwi na mambukizi kuendelea kutazamwa mpaka wanapotimiza miaka miwili au kuacha kunyonya na kwamba kwa kipindi cha Octoba-Disemba 2022 wamefanikiwa kufikia asilimia 85 ya watoto wanaozaliwa na akina mama wenye maambukizi wanaojifungua kwa mkoa mzima


“Watoto wanaozaliwa na akina mama wenye mambukizi tunawafuatilia na kuwafikia  mapema ili kujua hali zao,ambao hawajakutwa na maambukizi ya virusi tunaendelea kuwaangalia mpaka wanapotimiza miezi 18 au hadi watakapoachishwa kunyonya lengo ikiwa ni kuhakikisha hawapatwi na madhara yoyote” Amesema Ndossi


Akizungumzia hilo mkurugenzi mtendaji wa THPS Redemta Mbatia amesema kazi kubwa ya mradi wa Afya Hatua ni kuibua watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na  kuwaunganisha kwenye huduma endelevu na ambao hawakutwi na maambujizi wanapewa elimu ili kuhakikisha hawapati mambukizi kwa kutumia dawa kinga kutokana na hali hatarishi mtu aliyonayo.


Amesema mpaka sasa mkoa wa Kigoma umesajili watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI 25540 na kati yao asilimia 99 wametumia dawa na kufubaza virusi na kutoa wito kwa wanachi kutumia huduma za afya zinazotolewa na serikali pamoja na wadau ili kuhakikisha taifa linakuwa na watu wenye afya  kwaajili ya maendeleo endelevu.

 

“Tunaendelea kuangalia mazingira yanayoleteleza maambukizi ikiwemo ukatili wa kijinsia ambapo kwa mwaka jana  tumeweza kuibu visa 2500 vya ukatili wa kijinsia  na kutoa unasihi wa namna ya kujikinga wasipate maambukizi” Amesema Mbatia


Kwa upande wa Mageni Pondamali Mratibu wa UKIMWI wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu amesema wanashirikiana na THPS kutoa huduma katika vituo 15 vya upimaji na tiba ya VVU na kwamba hadi Disemba mwaka 2022 walifanikiwa kubaini wateja wapya 345 ambao tayari wapo kwenye matumizi ya dawa ya kufubaza virusi na kwamba jumla ya watu wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI ni 2525.


Naye Mohammed Abbas mraribu wa afya kutoka Redcross Tanzania amesema wamefanikiwa kugundua wateja 573 wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kwamba wengi wanaogundulika kuwa na virusi kambini huanza dawa siku ya kwanza kutokana na uhamasishaji unaofanyika. 


Abbas amezitaja changamoto kuwa ni baadhi ya wagonjwa kuacha kutumia dawa wakiamini kupona kwa njia ya maombi au dawa za kienyeji pamoja na upungufu wa vituo vya ushauri na tiba ambapo kwa kambi nzima vipo vituo tisa ambavyo vinne kati ya hivyo vinatoa huduma za chanjo na kimoja pekee kutoa huduma na kinga ya VVU na kuomba uongozi wa CDC kuwaongezea vituo viwili ili kuongeza huduma ombi ambalo limeahidiwa kufanyiwa kazi na mkurugenzi mtendaji wa THPS.

Post a Comment

0 Comments