TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAH. WABUNGE- WAZIRI KAIRUKI

Na Mwandishi Wetu, Katavi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki  amesema Ofisi yake ipo tayari na itaendelea kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge katika kutatua cuangamoto za wananchi.

Waziri Kairuki  amesema hayo leo tarehe 9 Februari, 2023  wakati alipokutana na Waheshimiwa Wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Katavi.

"Kikao hiki kitatupa  mwanga wa kujua Wabunge wanahitaji kupeleka nini kwa wananchi na kupitia mjadala huu tutapata mwelekeo  wa pamoja ili kuweza kutatua changamoto za  wananchi" amesema Kairuki.

Ameongeza lengo la kukutana na nanyi  ni kuhakikisha changamoto za wananchi zinawasilishwa na  Ofisi ya Raia TAMISEMI inazifanyia kazi.

"Huduma bora kwa wananchi wetu ni muhimu nasi tunaamini ninyi Waheshimiwa Wabunge ndio mtatusidia sababu ninyi  ndio wawakilishi wa wananchi"

Naye  Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mhe. Mbunge wa Katavi Isack Kamwele amemshukuru Waziri Kairuki na timu yake ya watendaji.

"Sisi kama  Wabunge wa Mkoa wa Katavi tutaendelea kutoa ushirikiano na Wizara ya Ofisi ya Rais-  TAMISEMI kwa kuendelea kuzisemea changamoto zinazowakabili wananchi kwani tunaamini  kwa pamaja tutaweza kutatua changamoto hususan za Elimumsingi, Afyamsingi, Miundombinu ya barabara na masuala ya kiutawala.

Post a Comment

0 Comments