WADAU WANAOTEKELEZA AFUA ZA AFYA WAKUTANA KUJADILI VIPAUMBELE KWA MWAKA 2023.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
Wizara ya Afya kupitia idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto, leo terehe 23 Februari, 2023 imekutana na kufanya mazungumzo na wadau wanaotekeleza afua za afya, mtoto mchanga, vijana na masuala ya ukatili wa kijinsia Ili kugundua vipaumbele katika utekelezaji wa Afua hizo Kwa mwaka 2023.

Akizungumza katika Kkikao kazi hicho  ambacho kimefanyika Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Watoto na Vijana Dkt. Felix Bundala amesema kikao hicho  kina lengo la kuja na makubaliano ya pamoja juu ya namna bora afua hizo zitatekelezwa kwa ajili ya manufaa kwa watanzania, hasa kupunguza vifo  vya watoto wachanga.

"Tuna lengo moja kubwa la kutathmini shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa ushirikiano huu wa wadau, hivyo washiriki wa kikao hiki watapata fursa kupitia makundi kujadili na kubaini mapungufu gani ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi."Amesema Dkt Bundala.

Pia Dkt Bundala amesema ni matarajio yetu baada ya kikao kazi hiki tutatoka na makubaliano ya pamoja juu ya vipaumbele na namna ya kuvitekeleza kufikia watanzania wote nchi nzima kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kikao kazi hicho kime hudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, vyama vya kitaaluma na wawakilishi mbali mbali kutoka vituo vya kutolea huduma za afya.

Post a Comment

0 Comments