WAFANYABIASHARA WALIA NA IDADI KUBWA YA MASOKO MANISPAA KIGOMA UJIJI

Na Mwajabu Hoza, Kigoma.
WAFANYABIASHARA katika soko la Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuondoa masoko holela ili kusaidia kuongeza mzunguko wa fedha katika soko hilo ambao kwa sasa umezorota na hivyo kuhatarisha mitaji yao.

Hayo yameelezwa na wafanyabiashara wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kali katika soko hilo na lengo la ziara hiyo ni kuangalia mazingira wanayofanyia biashara pamoja na kusikiliza maoni na kero walizonazo nyakati za ufanyaji wa biashara.

Tangu mwaka Jana wafanyabiashara walipopisha ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanga wafanya biashara wote walitakiwa kuingia katika soko la Masanga ambapo baadhi yao walihofia kushindwa kufanya biashara katika soko hilo na kukimbilia mitaani na wengie kuingia katika masoko yasiyo rasmi na hivyo kupunguza idadi ya wafanyabiashara katika soko la Masanga.

Wakizungumzia hilo baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Shamrat Manjinga na Ramadhan Mchondo wamesema kwa sasa kumeibuka masoko mengi ambayo yanachangia wafanyabiashara kutawanyika huku wateja ambao ndio watengemezi wao katika ununuzi wa bidhaa wakiwa ni wachache.

Mwajuma Rashidi ambaye anauza samaki wabichi katika soko hilo anasema mara kadhaa amekuwa akirudisha samaki nyumbani na mara nyingine kulazimika kuzikaanga na kuziuza kwenye masoko mengine na hilo linatokana na kukosa wateja ndani ya soko hilo.
 
Aidha wameiomba serikali kuangalia mambi kadhaa ikiwemo uanzishwaji holela wa masoko ndani ya Manispaa, masoko yasiyo rasmi yaweze kufungwa pamoja na wale waliotakiwa kuwa ndani ya soko la Masanga waweze kurudi.

Kilio kingine kinachowakabili wafanyabiashara hao ni kodi kubwa ya vibanda ambao wanaeleza imekuwa ni kikwazo kutokana na mauzo yao kuwa madogo ambapo hilo linachangia wafanyabiashara wengi kukimbilia mtaani na masoko mengine ambayo kodi ipo chini.

Kwa mujibu wa kaim Afisa biashara wa Manispaa Robert Sabuhoya amesema idadi ya wafanyabisha 862 walipaswa kuhamia katika soko Masanga lakini hadi sasa wapo takribani 400 na hivyo kuchochea mzunguko mdogo wa kibiashara.

Amesema hadi sasa Manispaa  inaendelea na ujenzi wa mabanda kwenye soko hilo pamoja na kuboresha maeneo ya wafanyabiashara wa mahindi ili waweze kuanza kuuza bidhaa zao ambao wao pia watachingia ongezeko la mzunguko wa biashara.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kali ambaye ametembelea soko hilo ametoa maagizo kwa mkurugenzi Manispaa ya Kigoma Ujiji kwanza kutazama upya kodi ya vibanda pamoja na kupunguza idadi ya masoko ambayo hayapo rasmi.

“Kama mwenyekiti wa soko alivyoomba vibanda vyote vijae watu na kufanya hivyo kutasaiidia kuongeza mzunguko wa fedha , si jambo zuri kila baada ya mita mia ama mia mbili kunakuwa na masoko mengi yanayofanana hakuna tija kinachotakiwa ni kuboresha masoko machache ili kuwe na tija” amesema. 

Post a Comment

0 Comments