WAKANDARASI WASIO NA TIJA HAWANA NAFASI

Na Mwajabu Hoza, Kigoma
MKUU wa wilaya ya Kigoma SALUM KALI amesema wakandarasi ambao watashindwa kutekeleza miradi kwa kuzingatia weledi na kukamilisha kwa wakati hawana nafasi katika wilaya hiyo.

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji amesema ni wakati sasa kuondokana na tabia ya mazoea katika utekelezaji wa miradi ambayo imekosa kuwa na tija kwa wananchi.

Amesema Wakandarasi wasio na tija kwa serekalii na wananchi ni kipaumbele chake namba moja kati ya vipaumbele vyake saba alivyoainisha ambapo amesisitiza kuwa wakandarasi hao hawatapata nafasi ya kula fedha ambazo ni kodi za Watanzania.

“Hatuwezi kuendelea na wakandarasi wasiojiweza miradi inasuasua unakwenda leo mara hayupo mara vifaa vimeharibika kumbe  anakodi hadi mitambo, sio kwenye utawala wangu lazima tusimamie kwa pamoja miradi imalizike kwa wakati na ubora wake uonekane.”

Pia akasisitiza suala la ukusanyaji wa mapato kuhakikisha mapato yanaongezeka  katika halmashauri kupitia vyanzo vilivyopo ikiwa ni pamoja na kuibua vyanzo vipya na kuwataka  watendaji kuhakikisha wanasimamia vyema katika maeneo yao.

“ Watendaji mpo hapa pesa mbichi hatuchukui haikubaliki lazima fedha ipitie kwenye mifumo “ aliesema

Kaimu Mkurugenzi  Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Jabili Timbako na Evans Mdee Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Kigoma Ujiji wamesema wao kama watendaji watahakikisha suala la wakandarasi linasimamiwa ipasavyo wakati wa upatikanaji wao.

Wamesema licha ya changamoto ndogondogo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo lakini wameendelea kufanya ufuatiliaji na kuboresha maeneo ambayo yameonekana kuwa na changamoto.

Post a Comment

0 Comments