WAKULIMA MICHIKICHI WADAI RUZUKU,WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATOA WASIWASI

Na Isaac Aron Isaac, Kigoma
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa amesema serikali itaendelea kutatua changamoto katika endelezaji wa zao la mchikichi ikiwemo kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa mitaji kwa wakulima na wadau ili kukabiliana na mahitaji ya tani laki sita za mafuta kwa mwaka nchini.
 
Ametoa kauli hiyo katika kikao cha tathimini ya zao hilo mkoani Kigoma kilichohusisha wadau wa tasnia ya zao hilo kutazama mafanikio na changamoto ambazo zinawakabili wakulima.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amesema ni wajibu wa serikali kuendelea kuwawezesha wadau na wakulima ili zaidi ya shilingi bilioni 400 zinazotumika kuagiza mafuta kutoka nje ziweze kutumika ndano ya nchi.
 
Kwa takribani miaka sita tangu harakati za kufufua zao hilo kuanza Mkoani Kigoma wakulima na wadau wanaeleza jitihada ambazo serikali imekuwa ikifanya ikiwemo utengenezaji wa mbegu za kisasa ambao hautakuwa na tija ikiwa serikali haitaweza kutenga ruzuku kwa wakulima kwaajili ya zao hilo.
 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde amesema changamoto hizo zinazowakabili wakulima na wadau zimeendelea kuathiri uzalishaji wa mafuta ya mawese kwani mahitaji kwa nchi ni asilimia 12 sawa na tani takribani laki tatu huku uwezo wa uzalishaji wa ndani ni asilimia 2 pekee.

Kwa sasa mkoa wa Kigoma unaongoza katika uzalishaji wa zao la mchikichi kwa asilimia 80 kote nchini ikifuatia na mikoa mingine ambayo hulima minazi.

Post a Comment

0 Comments