WATENDAJI KIGOMA WAAGIZWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO.

Na Kadislaus Ezekiel, Kigoma
Watendaji wa Kata katika Halmshauri ya wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, wameagizwa na kusisitizwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo yao ya kazi, na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Hamisi Kalli ametoa maelekezo hayo wakati akikabidhi pikipiki sita zilizotolewa na serikali kwa watendaji, huku akiwataka kuhakikisha wanatelekeza majukum yao kwa weredi, na kuhakikisha vyombo hivyo vinasaidia katika ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Rose Manumba amewataka watendaji hao kutotumia pikipiki hizo kama bodaboda na kwamba bado serikali itahakikisha watendaji wote wanapata vyombo hivyo vya usafiri.
 
Kwa upande wao baadhi ya watendaji wa Kata, wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo, wamesema zitakuwa chachu katika kurahisisha majukum yao kwa wakati na weredi.


Post a Comment

0 Comments