WAVUVI KIGOMA WAGAWIWA VIFAA VYA UVUVI VYENYE THAMANI YA TSH. MIL. 70.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amegawa vifaa vya uvuvi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 70 kwa wavuvi waliopo Forodha ya Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akigawa vifaa hivyo, mbali na kutoa shukrani kwa shirika la Afrika Relief Organization ambalo ndilo limenunua vifaa hivyo Mheshimiwa Andengenye amewataka wavuvi wa mkoani kigoma kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kupatiwa msaada.

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa ambaye alihamasisha shirika hilo kuwapatia msaada wavuvi hao na kuwataka wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia kwa usahihi ili kuondokana na umasikini.

Nao baaadhi ya viongozi wa shirika la Afrika Relief  Organizationi akiwemo Mkurugenzi wa shirika hilo  Dr Sammy Mohamed wamesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Post a Comment

0 Comments