WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA YA SONGWE

Na Mwandishi Wetu, Songwe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya ya Songwe.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha Mradi huu tarehe 31
machi 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo
tayari vifaa vyake vimepokelewa.

Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha Ujenzi wa Majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, Mionzi, Maabara, ufuaji, Famasia, Utawala na Jengo la Mama na Mtoto, Ujenzi wa Wodi tatu za Magonjwa Mchanganyiko.

Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (Wanaume na Wanawake)

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha hakuna eneo katika nchi hii ambao hapajatekelezwa miradi ya huduma za jamii kaunzia ngazi ya mkoa hadi kijiji.

Post a Comment

0 Comments