WAZIRI NAPE AIPONGEZA TAASISI YA WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI (TOMA)

Na Editha Karlo, Dodoma
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameipongeza klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha (APC) kwa kuanzisha taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni,Tanzania Online Media Alliance (TOMA).

Nape ametoa pongezi hizo februari 10, 2022 kwenye ukumbi wa Hotel ya Morena wakati wa hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na msemaji wa serikali na mkurugenzi wa habari maelezo Gerson Msigwa katika uzinduzi wa taasisi hiyo jijini Dodoma.

Waziri Nape ameutaka uongozi wa klabu ya waandishi wa habari Arusha (APC) kuendesha mafunzo ya weledi kwa waandishi wa habari mtandaoni kwani wengi hawafuati misingi ya uandishi wa habari.

Amesema sasa hivi vyombo vingi vya habari vya mtandaoni vinasumbuliwa na weledi lakini pia baadhi uzusha habari ambazo hazipo na kuzua taharuki kwenye jamii.

"Tunapaswa kujitofautisha ili tulinde taaluma yetu na serikali ina ona juhudi za vyombo vya habari ndo maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo chake"amesema Msigwa kwaniaba ya Nape Nnauye.

Amewaomba wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji wa kazi zao hasa katika kipindi hiki cha matumizi ya teknolojia kwa kuhakikisha wanazingatia maudhui yanayoendana na taaluma.

Aliwataka pia waandishi wa habari za mtandaoni kujiunga kwa wingi na taasisi ya TOMA ili waweze kunufaika na taasisi hiyo pia kuwa waandishi wenye weledi katika taaluma yao.

"Nimestuka kidogo taarifa yenu imesema mnawanachama 20 tu hii imenisikitisha, uchache huu Tanzania waandishi wapo wengi wanaoandika habari za mtandao niwaombe waandishi mjiuunge kwa wingi na taasisi hii"Amesema Msigwa

Naye mtendaji mkuu wa Taasisi ya Freedom House Tanzania, wakili Daniel Lema amesema kuanzishwa kwa TOMA ni matokeo ya mradi wa kuimarisha demokrasi nchini (DataDriven Advocacy) ambao ulikuwa chini ya ofisi yake na shirika la pact.

Amesema mradi huo ulikuwa ukifanywa na kusimamiwa na chama cha waandishi wa habari Arusha (APC) ambao umeleta manufaa makubwa kwa waandishi 20 waliokuwa wakitekeleza mradi huo ambapo wameweza kupatiwa mafunzo mbalimbali yanayoendama na taaluma yao pia baadhi yao wameweza kumiliki vyombo vyao mtandaoni, wengine wakipewa tunzo na serikali kwa kutambua kazi zao.

Naye Mwenyekiti wa Arusha Press Club ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya TOMA Claud Gwandu amesema taasisi hiyo imeanzishwa baada ya kuona uandishi wa mitandaoni unakua kwa kasi japo baadhi wanaripoti taarifa ambazo hazina weledi.

"Tumefungua milango ipo wazi wanachama wengi waje kujiung na TOMA, tutahakikisha taasisi yetu inakuwa na waandishi wenye weledi katika uandishi wao,tutawapa mafunzo ili kuwajengea uwezo kwenye kazi zao "Amesema Gwandu

Post a Comment

0 Comments