AFISA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KOSA LA UBAKAJI

Na Jacob Ruvilo, Kigoma
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemuhukumu kwenda jela miaka 30 Afisa ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Wilaya hiyo Frank Mabuga baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka 13.

Hukumu hiyo imesoma kwa takribani dakika 29 katika chumba cha siri  mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Eva Mushi.

Shauri hili lilitajwa kwa mara ya kwanza Februari 22 mwaka jana 2022 mbele ya Hakimu wa wilaya Venance Mwakitalu ambapo Frank alituhumiwa kumbaka mara mbili usiku kucha katika nyumba ya kulala wageni ya Ishimwe mnamo Desemba 19. 2021 nakumsababishia maumivu makali na michubuko sehemu za siri.

Muathiriwa wa ubakaji huo ni  mtoto wa kike miaka 13 ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mlole ambapo  alimrubuni kufanya nae mapenzi kinyume cha sheria ya mtoto.

Shauri hili lilikuwa na mashahidi sita upande wa Jamuhuri na vielelezo viwili huku hii leo upande wa mshitakwia alikuwepo wakili Ignatus Rweyemamu ambaye hata hivyo hakutaka kuzungumza chochote mara baada ya hukumu.

Hakimu mushi amefafanuwa kuwa hukumu hii nikwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo (1)(2)e na kifungu 131 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu namba 16@2019 na marekebisho yake ya mwaka 2022 na amemuhukumu kwenda jela  miaka 30,.

Wakili wa serikali Happiness Mayunga ameeleza kuridhishwa na hukumu hiyo nakwamba nivema watu waliopewa wadhama ya kulinda mtoto wawe mfano bora badala ya kuwa mstari wa mbele kuvunja sheria

Post a Comment

0 Comments