BILIONI 3 ZATENGWA NA SERIKALI KWAAJILI YA UJENZI WA SOKO LA MWANGA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI


Na Mwandishi Wetu, Kigoma.

Zaidi ya shilingi Bilioni 3 zimetengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa soko la Mwanga lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Ili kuinua uchumi wa Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amebainisha hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuongeza kuwa Serikali imetilia maanani katika kuhakikisha inaboresha mazingira  ya kufanya biashara.

Aidha Mkuu wa Wilaya huyo amesema katika kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unakua kiuchumi Serikali imetoa Zaidi ya Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Kigoma na zaidi ya Shilingi Milioni 22 za awali zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Meli ndani ya Ziwa Tanganyika

Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Wilaya ya Kigoma wamesema juhudi za kufanya biashara zimekuwa zikirudi nyuma kwa sababu ya sheria kandamizi pamoja na utaratibu usio mzuri wa Masoko ya kufanyia biashara.

Post a Comment

0 Comments