WATENDAJI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUONGEZA KASI UZALISHAJI ZAO LA MICHIKICHI

Na Mwandishi Wetu, Uvinza

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewataka watendaji wa Halimashauri ya Wilaya kushirikiana na taasisi za Wizara ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao la mchikichi wilayani Uvinza ambako zao hilo linalimwa kwa wingi Katika Mkoa wa Kigoma.

Dkt. Hashil ameyasema hayo Machi 27, 2023 Mkoani Kigoma alipotembelea Wilaya ya Uvinza na kufanya kikao na Mkuu wa Wilaya Mhe. Dinah Mathaman Chenye lengo la kufuatilia maelekezo ya Mhe Waziri Mkuu kuhusu maombi va mwekezaii wa kiwanda cha TROLLE MEES LE TANZANIA IS LTD kupatiwa ardhi kwa ajili ya kilimo cha mchikichi Wilayani Uvinza ili kuongeza malighafi katika kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji.

Nae Mhe. Dinah Mathaman Mkuu wa Wilaya ya Uvinza amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara yake, na kusema kuwa itaongeza chachu kuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi shirikishi kwa ushirikishwaji wa taasisi zilizo chini ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika Wilaya ya Uvinza. 

"Katibu Mku umefanva jambo jema kuja na watendaji wako wakuu kutoka SIDO, WMA, TIRDO, CAMARTEC a TBS kazi zetu hapa wilayani tunahitaji ushirikiano kwenye utekelezaji wake hasa katika shughuli za vipimo, unazo taasisi kama WMA na SIDO amabao watatusaidia katika teknolojia ya kisasa na ili kupata zana za kilimo na mitambo ya kisasa ya kusindika mazao yetu" amesema Mhe, Dinah.

Halikadhalika Dkt. Hashill alitembelea Kiwanda Cha Nyanza mane Tanganyika Ltd cha kuzalisha chumvi kilichopo Wilayani Uvinza, lengo la ziara hiyo ni kutaka kujua Changamoto zilizopo na kuzitatua.

"Miezi mitatu nyuma tulipata Changamoto kidogo ya zao la chumvi, kwa hiyo tulifanya ziara kubwa kwa kushirikiana na Wizara ya Madini, tulienda mikoa ya kusini ikiwemo Mtwara na Lindi na kutoa baadhi ya matamko, lakini tulipo toa matamko tukapata mwekezaji mmoja anatoka Uvinza akaja akanieleza kuwa, mimi kwangu kuna matatizo kidogo tofauti na haya, hivyo akawa ameomba nimtembele siku moja ndiyo maana nimekuja kujua changamoto mlizonazo hapa Nyanza Mine " Amesema Dkt. Hashill.

Bornny Mwaipopo ambaye ni Meneja wa kiwanda cha Nyanza mane Tanganyika Ltd amemshukuru Katibu Mkuu kwa kufanya ziara kiwandani hapo.

Post a Comment

0 Comments