IDADI YA WAOMBA HIFADHI KUTOKA DR CONGO WALIONGIA KIGOMA YAFIKIA 6021

Na Isaac Aron Isaac, Kigoma.
Idadi ya waomba hifadhi kutoka nchi ya Congo DRC kuingia Mkoani Kigoma imefikia 6021 ambapo Watoto na wanawake wakitajwa kuwa wengi zaidi.
 
Akizungumza na wanahabari mratibu wa kanda ya magharabi idara ya kuhudumia wakimbizi Nashoni Makundi amesema kwa sasa kila siku karibu watu 100 hadi 200 huingia nchini kutoka maeneo ya Goma,Baraka na kivu kaskazini.

Idara ya kuhudumia wakimbizi imeeleza kuimarisha ulinzi katika maeneo ya vijiji vya kusini na kaskazini mwa Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma ambapo ndio maeneo ambayo wengi hupita kuingia nchini.

Licha ya idadi ya wale wanaongia nchini kupungua kutoka 300 hadi 600 kwa siku hadi 100 na 200 baadhi ya raia wa Congo DRC wanasema hali sio shwari kwani mauaji na vitendi vingine bado vinaendelea.
 
Kati ya watu 6021 ambao wameingia nchini kuomba hifadhi 50 kati yao wamebainika kuwa ni Watanzania ambao walikuwa wakiishi nchini Congo DRC.

Post a Comment

0 Comments