Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Serikali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Saalam wameanza kampeni ya usafi wa mazingira kwenye mialo na fukwe za ziwa Tanganyika
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Saalam Bahati Bayoma amesema wamefanya kampeni hiyo kwa sababu hadi kufikia mwishoni mwa Mwaka 2022 takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa tani milioni 8 za taka za plastiki zinazozalishwa duniani zinaingia kwenye vyanzo vya maji.
Naye Afisa Usafi na Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Petronia Gwakila amesema kampeni hiyo inamanufaa kwani itafanya mazingira kuwa masafi, huku akiwataka wavuvi na wananchi kutilia maanani suala la usafi wa mazingira kwenye maeneo wanayoishi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bangwe Said Betese akiwa na baadhi na viongozi wa wavuvi katika Mwalo wa Katonga wamesema mazingira yanapokuwa masafi yanasaidia kutokuwepo kwa mlipuko wa magonjwa hasa kipindupindu.
0 Comments