SERIKALI YATOA SIKU 21 KUBADILISHA TAHASUSI (COMBINATION) KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2022

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
SERIKALI imetoa siku 21 kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana  kubadili tahasusi na kozi za vyuo vya kati  ili kufanya chaguzi sahihi.

Hayo yamesemwa na  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Charles Msonde leo Machi 14,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa ya kubadili Tahasusi kwa wanafunzi  waliomaliza kidato cha nne mwaka 2022

Amesema kuwa Serikali imetoa fursa hiyo kutokana na baadhi ya wanafunzi  walifanya chaguzi awali kuwa na mitazamo tofauti ambayo inahitaji kufanya marekebisho baada ya matokeo kutoka Januari 19.

“Wajibu wa TAMISEMI ni kuwapangia shule au vyuo mbalimbali ili kuanza masomo Julai mwaka huu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta, ili hili lifanyike lazima wawe wamefanya machaguo yao wanayotaka kusoma, vyuo au shule na fani gani wanazipenda ,”amesema Dkt. Msonde.

Amesema Serikali imewapa fursa wanafunzi hawa kufanya marekebisho ya tahasusi zao kama inafaa, lengo ni kufanya chaguzi sahihi kadiri walivyofaulu, baada ya hapo tutaamua kupitia chaguzi walizofanya, lakini kwaa wale waliochagua sahihi awali na kuona ni sahihi tangazo hili haliwahusu

“Tunatoa fursa inawezekana baada ya matokeo ameona mtazamo mwingine anahitaji kufanya marekebisho, au anataka kusoma kitu kingine badala ya alichochagu, hivyo tunatoa siku 21 kuanzia leo maana mfumo utakuwa wazi zoezi litaisha Aprili 6 tunaamini kipindi hichi kinatosha kufanya marekebisho.”amesema.

Dk. Msonde ametoa a rai kwa wanafunzi kufanya marekebisho kama ni lazima kufanya hivyo maana hakutakuwa na mabadiliko mengine baada ya wiki tatu(siku 21)kuisha.

Aidha, amewataka kufanya uchaguzi kwa kuzingatia ufaulu wa masomo kwa sababu utakuwa wa ushindani kwenye tahasusi zilizochaguliwa.

“Hakikisha unachagua masomo unayoweza ili usichague nyingine ukashindwa ukakosa.”alisisitiza.

Pia, amewashauri wanafunzi kushirikisha wazazi, walezi na walimu kuhusu namna ya kufanya chaguzi za tahasusi ili iwasaide kuchagua wanachokipenda kulingana na ufauli.

Post a Comment

0 Comments