VIJANA KIGOMA KUNUFAIKA NA MRADI WA AFYA YANGU MAENDELEO YANGU


Na Mwansishi Wetu, Kigoma

Kutokana na Vijana kuwa kundi muhimu sana katika maendeleo ya familia na taifa, Jamii kwa ujumla imetakiwa kuhakikisha inawasimamia vijana kupata Elimu, Ujuzi na taarifa kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo afya yao ili waweze kunufaika na uwekezaji unaofanywa na serikali pamoja na mashirika mbalimbali kwa lengo la kumletea maendeleo kijana.

Haya yanajiri baada ya Shirika la Maendeleo ya Vijana KIVIDEA lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji kuzindua mradi wa "Afya Yangu Maendeleo Yangu" unaolenga kumsaidia kija a kupata stadi za maisha na kumuongezea maarifa yatakayomsaidia kijana kufikia maendeleo yake.

Akizungumza katika uzinduzu huo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Msafiri Nzunuri, ambaye ndie alikuwa mgenu rasmi amelipongeza shirika la KIVIDEA kwa kuanzisha mradi huo ambao unaenda sawa na sera ya maendeo ya vijana ya mwaka 2007 ambayo imeainisha mahitaji ya Vijana ili kuleta mchango katika masuala ya maendeleo.

"Vijana ni kundi ambalo ni muhimu sana katika jamii hivyo wanatakiwa kuandaliwa vizuri, kusimamiwa vizuri na kufuatiliwa ili baadae tuwe na vijana wanaojitambua na wanaoweza kupambana na changamoto za ukatili au zile ambazo zitahatarisha afya zao.

"Kama kuna mambo ambayo wazazi hawafanyi ya kumsaidia huyu mtoto na kama usimamizi ngazi ya familia hautaimalishwa inawezekana uwekezaji mkubwa unaofanywa usilete matokeo yaliyokusudiwa" amesema Nzunuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Maendeleo ya Vijana KIVIDEA Babu Paschal Steven amesema mradi wa Afya yangu maendedeleo yangu umewalenga vijana na watoto ili kuwasaidia kukua katika malezi sahihi na kujua namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo kutoa taarifa ya vitendo hivyo.

"Kwa vijana mradi huu unaenda kuwaongezwa maara zaidi katika kukabiliana na changamoto za kila siku, ndio mana mradi huu unasisitiza kwamba vijana wapewe elimu ya stadi za maisha, elimu ya afya ya uzazi na elimu ya kupinga ukatili kwasababu tunajua kwamba changamoto za ka siku za vijana pamoja na makundi rika, ili kijana aweze kukabiliana na shinikizo rika lazima awe na elimu ya kujitambua, ajijue yeye ni nani na yuko kwenye changamoto gani na aweze kukabiliana nazo vipi" amesema Babu Paschal.

Nae Jackline Kitema ambaye ni Meneja wa Mradi huo amefafanua namna mradi huo utakavyofanya kazi kwa vijana kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji na Wilaya ya Uvinza ambao ndio wamelengwa kupatiwa elimu ya afya ya Uzazi, ukatili wa Kijinsia na Stadi za maisha.

Amesema mradi umelenga vijana kuanzia miaka 15 mpaka 24 ambapo watakuwa na klabu mashuleni katika shule za sekondari saba na shule za  msingi tatu na kila klabu itakuwa na vijana 30 Ili kuwafikishia elimu.

"Lakini pia tunafanya shughuri za watoto kuanzia miaka 8 hadi 14 kwasababu mtoto ukianza kumpa elimu akiwa mdogo anaelewa zaidi, na watoto wanaoishi katika mazingira magumu watapatiwa mahitaji yao ya kiutu na kielimu ikiweno Bima ya Afya" amesema Bi Kitema.

Akizungumzia Mradi huo Kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dkt Tibezuka Zinga amesema mradi huo utakuja kuwasadia watoto katika makuzi yao huku akiwashauri wazazi kutoa ushauri kwa wataalamu ili kufanikisha lengo la mradi.

"Malengo ya mradi ni mazuri kwasababu watoto wengi katika jamiii yetu wamepata madhara makubwa kulingana na jamii yetu kuwa na mabadiriko makubwa lakini jamii inatakiwa sasa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wakati wanapotembelea maeneo mbalimbali kutoa elimu kwa watoto ambao ndio taifa la Kesho."

Kikao hicho cha uzinduzi wa mradi wa Afya Yangu Maendeleo Yangu kilihudhuliwa na wataalamu kutoma Sekta ya afya na Elimu, maafisa maendeleo ya jamii ikiwemo maafisa Ustawi wa jamii mkoani Kigoma.

Post a Comment

0 Comments