VIONGOZI KIGOMA WAMETAKIWA KUSIMAMIA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA


Na Emmanuel Matinde, Kigoma

Viongozi wa Halmashauri zote mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia ipasavyo vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze kukusanya mapato ya kutosha kununulia bidhaa za afya ili kuhakikisha huduma za matibabu kwa wananchi zinapatikana muda wote bila manung’uniko.


Mwaka 2018 serikali kwa kushirikiana na wadau ilianzisha mfumo unaoitwa MSHITIRI unaoruhusu vituo afya, zahanati na hospitali za Wilaya kununua dawa na vifaa tiba kupitia mzabuni mahsusi aliyependekezwa ili kufidia ombwe la ukosefu wa dawa zile ambazo hazipatikani Bohari Kuu ya Dawa MSD kwa wakati husika.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika mafunzo kwa watumishi wa idara ya afya ngazi ya halmashauri, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Uchumi na Uwezeshaji Ntime Mwalyambi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Jesca Lebba, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia mkoa wa Kigoma bajeti ya kutosha kwenye dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi lakini haitakuwa na maana kama mfumo wa MSHITIRI hautafanya kazi vizuri na kuwezesha wananchi kupata huduma.

Naye Mwezeshaji wa ngazi ya Taifa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mambo Gunze, amezungumzia umuhimu wa kutumia mfumo huo ambao kwa sasa unafanyika kwa njia ya mtandao.

Post a Comment

0 Comments