WAFANYABIASHARA 9 WAKAMATWA KWA KUKIUKA AGIZO LA WAZIRI MKUU


Na Kadislaus Ezekiel, Kigoma

Wafanyabiashara 9 wa mafuta ya mawese mkoani Kigoma, wamekamatwa na madumu  289 aina ya bidoo ambayo yalizidi uzito wa vipimo halisi wa lita ishirini,  ikiwa ni wiki kadhaa tangu Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kupiga marufuku vipimo hivyo nakuagiza vyombo vya dora kudhibiti jambo hilo.

Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoani Kigoma Laurenti Kabikie amesema watu hao wamekamatwa kufuatia taarifa za wasamalia wema ambapo wafanyabiashara hao walikuwa na gari aina ya fuso wakibeba madumu ya lita therathini ikiwa ni kinyume na maelekezo ya sasa.

"Tuna mafuta haya ambayo yako kwenye madumu ambayo hayana sifa, unaweza kuona inavyotulazimu kuangalia utaratibu wa kuweza kuyabinafsisha lakini kwakuwa tunafanya kazi na mamlaka zingine kama TBS na mamlaka zinazohusika kuangalia usalama wa chakula, tutashirikiana nao ili kuona njia itakayofa ili kujua mizigo hii itakwenda wapi" amesema Kabikie.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara waliokubwa na suala hilo akiwemo Febrick Leonard na Agnes Pius wamekili kuendelea kutumia bido kwa kudai kukosa weredi na kuiomba serikali itoe muda wa mpito wakati elimu ikiendelea kutolewa kwa wafanyabiashara.

"Baada ya hapo tulisubiri kuona serikali kama itatupa maelekezo vipimo vinavyohitajika ili tuvitumie, na haya madumu wanayosema yana lemikali huwa tukiyachukua tunayaosha na sabuni na maji ya moto ndio tunayawekea mawese" wamesema wafanyabiashara hao.

Post a Comment

0 Comments