WHO YAUNGA MKONO JUHUDI ZA KUTOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO KIGOMA

ᴺᵃ ᴰⁱᵃⁿᵃᴿᵘᵇᵃⁿᵍᵘᵏᵃ, ᴷⁱᵍᵒᵐᵃ.
Shirika la afya duniani (WHO) limetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa idara ya afya ya mkoa wa Kigoma kwa lengo la kutibu maji ili kuzuia magonjwa yatokananyo na uchafuzi wa maji ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine ya kuhara.

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na boksi 50 za vidonge vya kutibu maji, vifaa vya kupima kiwango cha vidonge vilivyopo kwenye maji 100, vifaa vya kupulizia dawa na vitakasa mikono 42 pamoja na vipeperushi 1000.
 
 Akizungumza hilo Dkt. Jairos Hiliza  ambaye ni Afisa wa shirika la Afya la kimataifa WHO Mkoa wa Kigoma amesema vifaa hivyo vimetolewa ili kuweka tahadhali ya kuwakinga wananchi na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafuzi wa maji hasa kwa kipindi hiki cha mvua ambapo magojwa ya mlipuko yanaweza kutokea muda wowote.
 
Naye mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dkt.Jesca Lebba  amesema  msaada huo umetolewa kwa wakati muafaka na kulishukuru shirika la kwa WHO kuendelea kutoa msaada wenye  lengo la kukabilana na magonjwa ambayo ni hatari kwa jamii nzima na kwamba vifaa hivyo vitagawiwa katika halmashuri zote tisa za mkoa.

iasaidia kukabili magonjwa ya mlipuko na magonjwa ya matumbo ambayo hutokea mara kwa mara kutokana na uchafuzi wa mazingira unaojitokeza hasa wakati wa mvua za mfurulizo.
 
"msaada umekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa wakati huu wa mvua changamoto ya uchafuzi wa mazingira  na vyanzo vya maji ni mkubwa na unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hasa kipindupindu na kuhara hivyo upatikanaji wa madawa hayo utasaidia kutibu maji na kuyafanya kuwa safi na salama kwa matumizi" amesema Dkt. Lebba

Post a Comment

0 Comments