KIGOMA BADO INA KIWANGO CHA JUU CHA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA


Na James Jovin, Kigoma

Mkoa wa Kigoma Bado unatajwa kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria licha ya kufanikiwa kupunguza maambukizi kwa aslimia 12 kutoka asilimia 24 mwaka 2017.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Ibrahimu Salehe wakati akitoa taarifa ya maambukizi ya Ugonjwa huo katika maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Kibondo.

Amesema kupungua kwa maambukizi hayo kumechangiwa na afua mbalimbali zilizofanyika ikiwa ni pamoja na kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani pamoja na ugawaji wa vyandarua mashuleni.

Licha ya jitihada hizo za serikali katika kutokomeza ugonjwa huo wilaya ya Kibondo imetajwa kuendelea kuwa na maambukizi ya juu ya ugonjwa wa malaria ambapo inaongoza kwa maambukizi kwaa silimia 23.9 huku manispaa ya kigoma ujiji ikiwa na kiwango cha chini kwa asilimia 6.8

Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye aliye wakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali Aggrey Magwaza katika maadhimisho hayo amewaagiza wakurugenzi katika Halmashauri za mkoa wa Kigoma kutenga Bajeti kwa ajili ya afua mbalimbali za kupambana na Ugonjwa wa malaria .

Post a Comment

0 Comments