MICHE ZAIDI YA LAKI 2 NA MIKOPO YA TSH. MIL. 600 VYATOLEWA KWA WAKULIMA KIGOMA


Na Emmanuel Matinde, Kigoma

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imeendelea kutekeleza agizo la serikali la kukuza zao la mchikichi kwa kuendelea kugawa miche ambapo miche zaidi ya laki mbili imegawiwa kwa wananchi sanjari na kutoa mikopo ya Shilingi Milioni 600 kwa vikundi vya wakulima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Rose Manumba, amesema jumla ya vikundi 6 vimepatiwa mikopo hiyo Pamoja na elimu ya ulimaji wa kisasa na kuondoa miche ya zamani ambayo imekuwa ikitoa kiasi kidogo cha mafuta.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli, amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa ya zao hilo huku akiwaalika wawekezaji wengine wenye nia ya kulima na kujenga viwanda vya kuchakata mafuta akiwahakikishia mazingira bora yatakayowezesha kuchochea ukuaji wa kilimo cha zao la michikichi.

Katika hatua nyingine Halmashuri ya Wilaya ya Kigoma imepanda miti zaidi ya laki tano kwa ajili ya kutunza mazingira ambapo zoezi hilo limefanyika katika Shule ya Msingi Msimba ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments