MIKOA 9 YAFANYA VYEMA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam
Mikoa 9 nchini imefanikiwa kushusha kiwango cha mamabukizi ya ugonjwa wa Malaria hadi kufikia chini ya asilimia 1 hivyo kufanya asilimia ya watu wanaoishi katika maeneo yenye malaria chini ya asilimia moja kufika 41%.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. @UmmyMwalimu kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa imeadhimishwa Jijini Dar Es Salaam.

Waziri Ummy ametaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Singida, Iringa, Dar es Salaam, Songwe na Mwanza kufanya idadi ya Mikoa hiyo kuwa 9 hadi sasa kutoka takwimu za Mikoa 6 ya mwaka 2017.

“Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya tunaendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuteleleza afua mbalimbali za kibunifu katika mapambano dhidi ya Malaria na tumeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria hadi kufikia chini ya asilimia 1” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Waziri Ummy amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kufikia Zero Malaria ifikapo mwaka 2030 ila kwa mikoa hiyo 9 inayofanya vyema, Serikali imeweka lengo la Zero Malaria ifikapo mwaka 2025.

Kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa huo Kitaifa, Waziri Unmy amesema Serikali imepiga hatua kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo na na kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kutoka asilimi 14.8 mwaka 2015 hafi kufikia asilimia 8.1 mpaka sasa.

“Tunaendelea kuwahimiza wananchi kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya endapo watahisi dalili za ugonjwa wa malaria ili kufanya vipimo na kupata tiba sahihi, sio kila homa ni malaria” amesema Waziri Ummy huku akiwataka wananchi kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa huo kwa kulala kwenye chandarua na kuweka mazingira safi ili kuangamiza mazalia ya mdudu mbu.

Post a Comment

0 Comments