RAIS AKUTANA NA MTOTO MWENYE MATATIZO YA NGOZI

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera. 

Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. 

Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments