RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA MAIMAMU NA MAAMUMA KIGOMA.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Mkono wa Eid Al-Fitr kwa Maimamu na Maamuma Mkoani Kigoma ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwaniaba yake na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye katika Msikiti wa Masjid Muumin Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Mara baada ya kupokea Zawadi hizo, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Haasan Idd Kiburwa ametoa Shukurani za dhati kwa Mhe. Rais Samia kwa kuguswa na kuamua kusherehekea Sikukuu hiyo pamoja na wahitaji Mkoani Kigoma.

Zawadi zilizotolewa na Mhe. Rais ni Mchele Kilo Mia moja, mbuzi wanne, Lita 40 za Mafuta ya Kula, Kilo 40 za Sukari, 50 za Maharage pamoja na 50 za unga wa Ngano.


Post a Comment

0 Comments