RAIS SAMIA AONGEZA BILIONI 5 HUDUMA ZA UBINGWA NA UBINGWA BOBEZI BILA MALIPO


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Katika kuunga mkono huduma za matibabu ya ubingwa bobezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza shilingi bilioni 5 kwenye bajeti ya Wizara ya Afya kwa ajili ya kugharamia huduma za ubingwa na ubingwa bobezi bure kwa Watanzania.

Akitolea mfano, Waziri  Ummy amesema,  fedha hizo angalau zitaweza kuwatibu watoto wenye Selimundi (Sickle Cell) wapatao 100 au  watakaopandikizwa figo 30 na kutakuwa na vigezo nani atapaswa kupatiwa huduma hiyo.

Waziri Ummy ameeleza hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma. 


Post a Comment

0 Comments