WAFANYABIASHARA KIGOMA WASHAURIWA KUJISAJILI ILI WAWE NA SIFA ZA KUPATA MIKOPO

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wametakiwa kufika katika maonyesho ya kuwawezwaha wananchi kiuchumi ili wapatiwe usajili utakao warahisishia kupata mikopo kwenye Taasisi zilizosajiliwa kutoa huduma hiyo.

Akizungumza katika viwanja vya Mwanga Community Center Manispaa ya Kigoma ambako ndiko yanafanyika maonyesho hayo, Afisa Usajili kutoka Brela Stanslaus Kisigo amesema wafanyabiashara wengi hawana sifa za kupata mikopo kwasababu ya kutosajiliwa.

"Unakuta mfanyabishara anahitaji mkopo ili kuongeza bishara yake lakini akienda kwenye Taasisi za mikopo anaonekana hana sifa hivyo wanashindwa kumsaidia" amesema Kisigo.

Katika upande mwingine baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali wadogo waliofika katika viwanja hivyo kwaajili ya maonesho wamelalamikia mwitikio mdogo wa wakazi mkoani humo kufika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupatiwa huduma.

"Kumekuja na bidhaa zetu ila shida muitikio, Wananchi wa hapa Kigom ni wachache sana wanaokuja kutazama na kuulizia bidhaa, kuwa muda tunakaa tu kwenye mabanda yetu bila kupata wateja" wamesema.

Maonesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi siku ya jumatatu yanalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na yanatarajia kufikia kilele tarehe 27 mwezi huu ambapo yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Uwezeshaji kiuchumi kupitia mabadiliko ya kidijitali".

Post a Comment

0 Comments