WANAHABARI WAPEWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA KATIKA KAZI ZAO.

 Na Editha Karlo,Tabora
CHAMA cha waandishi wa habari wanawake(TAMWA)kimefanya mafunzo ya siku moja kwa wanahabari zaidi ya 20 kuhusu ulinzi na usalama katika kazi zao.

Akifungua mafunzo hayo Meneja miradi na mikakati kutoka TAMWA  Sylivia Daulinge amesema kuwa usalama kwa wanahabari pamoja na vifaa vyao vya kazi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi ni jambo l msingi.

Hivyo ilikufanikisha majukumu yao ya kazi aliwataka wanahabari kuchukua tahadhali ya viashiria vyovyote ambavyo zinaweza kuhatarisha maisha yao ikiwemo kupoteza vifaa vya kazi.

"Mradi wetu huu ni wa miaka minne na huu ni mwaka watatu, Lengo la mafunzo haya ya siku moja ni kuwajengea uwezo, uelewa na kuwapa mbinu za kutambua hatari zilizopo mbeleni yenu mnapokuwa kazini na namna ya kujikinga nazo"Amesema Sylivia.

Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza Press Club amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwasababu hivi sasa kumekuwa na ongezeko la matukio mabaya kwa waandishi wa habari na kukosekana kwa mifumo imara ya ya kuwalinda.

Soko amesema kuwa wanahabari wanapaswa kutambua mazingira wanayofanyia kazi si salama hivyo wanapaswa kuchukua hatua ili kupunguza matukio ya ambayo siyo mazuri yanayoweza kuwakuta wakati wakitekeleza majukumu yao.

"Wanahabari wanapata changamoto za mauaji,kutekwa,kuteswa,kudhalilishwa,kunyang'anywa vifaa vya kazi,vitisho na mengine mnapokutana na changamoto hizo muwe mnatoa taarifa kwa kwenye vyombo vyenu na mamlaka zingine"Amesema Soko

Mwezeshaji aliongeza kwa kusema kuna aina mbili za usalama ambazo ni usalama wa mtu binafsi na vitu na usalama kimtandao hivyo akamtaka kila mmoja kuhakikisha anajilinda, kulinda vifaa vyake vya kazi na kuwa makini anapotumia mitandao.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa Shinyanga Suzan Butondo amewapongeza TAMWA kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waandishi kutoka Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Tabora, Simiyu na Singida kwani yatawasaidia kuchukua tahadhari wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

"Mafunzo haya ni muhimu kwetu kwasababu sasa hivi mitandao ya kijamii imechukua nafasi kubwa kwenye kuhabarisha umma kwa wakati hivyo usalama unahitajika ili kuweza kufanya kazi kwa weledi na usalama zaidi"amesema.

Post a Comment

0 Comments