HALIMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO YAPOKEA HATI SAFI KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA

Na Mwandishi Wetu, Kibondo
Halimashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imepokea hati safi katika maswala ya usimamizi wa fedha kwa mara ya saba Mfurulizo baada ya ukaguzi wa mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG kujilidhisha kuwa fedha mbali mbali za miradi ya maendeleo zinatumika vizuri kwa zaidi ya asilimia 90 ndani ya halimashauri hiyo.

Hayo yameelezwa na mweka hazina wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Shabani Kija wakati akiwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa IOM mjini Kibondo.

Aidha licha ya kupokea hati safi amesema kuwa kulinganga na taarifa za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali hoja za miaka ya nyuma zenye mashaka katika hesabu hizo zilikuwa zimebakia 96 ambapo zilifanyiwa kazi na kubakia hoja 26 pekee

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishina jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto Thobias Andengenye amesema kuwa licha ya halimashauri ya wilaya ya Kibondo kupata hati safi lakini mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali aligundua kuwepo na mapungufu mbali mbali ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi

Aidha mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amekili kupokea mapungufu hayo na kwamba yatafanyiwa kazi kwa masirahi ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha viongozi wote ndani ya wilaya hiyo wanafanya kazi kwa uadilifu kama ilivyo katika viapo vyao.

Honest Muya ambaye ni mkaguzi wa hesabu za serikali kutoka ofisi ya CAG amewataka viongozi wote ndani ya halimashauri ya wilaya ya Kibondo kuzingatia sana maadili katika shughuli zao ili kuepuka ubadhilifu wa mali ya umma unaoweza kusababisha halimashauri kupokea hati yenye mashaka na kukwamisha shughuli za maendeleo.

Post a Comment

0 Comments