RC ANDENGENYE AFUNGUA MIKUTANO BARAZA MAALUM (CAG) KASULU TC NA DC

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Katika kuhakikisha Halmashauri mkoani hapa zinapata ufumbuzi wa kudumu dhidi ya hoja mbalimbali za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali zinazojitokeza na ambazo zinaweza kuepukika, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye ameuagiza Uongozi katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuboresha Mfumo wa utunzaji wa nyaraka zikiwemo Hati za malipo ya Fedha ili kurahisisha upatikanaji wake pale zinapohitajika kwa ajili ya kujibu hoja hizo.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewaelekeza wakuu wa Vitengo vya Fedha na Biashara pamoja na Ugavi kutoa ushirkiano wa karibu kwa wakaguzi wa ndani katika Halmashauri ili kubaini Hoja hizo mapema na kuzitafuatia Ufumbuzi kwa pamoja.

Juni 13, 2023 Mkuu wa Mkoa amefungua na kushiriki Mikutano ya Mabaraza Maalum ya kupokea na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 katika Halmashauri ya Mji na Wilaya Kasulu.

Kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 Halmashauri hizo zimefanikiwa kupata Hati Safi za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali.

Post a Comment

0 Comments