RC ANDENGENYE ATOA WITO WA KUPUUZWA WANAOPOTOSHA KUHUSU HALI ZA BARABARA KIGOMA

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameutaka Umma wa Watanzania kupuuza Taarifa zinazosambaa katika Mitandao ya kijamii zikitafsiri uwepo wa Miundombinu ya Barabara isiyo rafiki mkoani Kigoma. 

Wito huo ameutoa Juni 15,2023 alipozungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia Majibu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 katika Halmashauri ya Buhigwe.

Siku za hivi karibuni Picha za watu wakiwa wamechafuka kwa vumbi huku zikiwa na maandishi yanayowatambulisha kuwa ni watumishi wapya wa Serikali waliopangiwa vituo vipya vya kazi na kuripoti mkoani hapa, zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha uwepo wa hisia tofauti kwa baadhi ya watu kuhusu uhalisia wa hali za Barabara katika Mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments