TBS YAKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH MIL 19

Na Kadislaus Ezekiel, Kigoma
SHIRIKA la viwango Tanzania TBS kanda ya Magharibi limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwenye maeneo ya biashara na kukamata bidhaa mbalimbali zilizopigwa marufuku zenye thamani ya zaidi ya milioni kumi na tisa zikiwemo nguo za ndani, Soksi na mafuta ya Braki za magari.

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi huo, Kaimu meneja TBS Kanda ya magharibi Elisha Meshack amewataka wafanyabiashara kutokiuka sheria ili kulinda usalama wa watumiaji.

Akizungumzia athali zitokanazo na matumizi ya vitu hivyo Bwana Meshack amesema watu watakuwa katika hatari ya kupata magonjwa ikiwemo magonjwa ya ngozi, hasa kwa watumiaji wa nguo za ndani zilizokwisha tumika.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wameomba elimu itolewe kabla ya bidhaa hizo kuingizwa sokoni, na kudhibiti wafanyabiashara wakubwa wanao ingiza bidhaa ambazo zilipigwa marufuku.

Post a Comment

0 Comments