VIJANA MKOANI KIGOMA SASA KUNUFAIKA NA FULSA ZILIZOPO

Na Diana Rubanguka, Kigoma
Vijana mkoani Kigoma wanatarajia kunufaika na fulsa mbalimbali zilizopo mkoani humo baada ya Taasisi ya Chemba ya wakulima,  wafanyabiashara na wenye viwanda (TCCIA) na VEVA Art And Craft  Kuungana kwa lengo la kuwainua vijana kiuchumi ili kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa ujumla.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa utiaji saini wa makubaliano baina ya taasisi hizo mbili, mwenyekiti wa TCCIA Abdul Mwilina alisema lengo kubwa la ushirikiano huo ni kuwainua vijana kiuchumi kupitia kilimo, biashara na viwanda kwani vijana ndio nguvu kazi katika maendeleo ya Taifa.
 
Mwilima amesema,  kumekuwa na wimbi kubwa la vijana ambao huziona fulasa na hata wakiziona fulsa hawajui namna ya kuzitumia huku akibainisha kuwa ushirikiano huo utagusa wilaya za Mkoa wa Kigoma
 
"Fulsa ni nyingi lakini vijana hawazioni, tuna wasomi ambao wamemaliza vyuo wanaosubiri ajira, tuna vijana waliopo mtaani pia hawana kazi za kufanya huku wakiwa hatumii fulsa ya katika mipaka ya nchi za Burundi na Democrasia ya Kongo" alisema Mwilima.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa  VEVA Art And Craft Genoveva Mtiti  amesema katika ushirikiano baina ya TCCIA na VEVA watakuwa na utaratibu wa kuwafikia vijana kwakuwafuata maeneo walipo na kuwapa kwa kuwafanyia mafunzo ya namna ya kupata mawazo ya kibiashara ili kufikia lengo lao la kuondokana na vijana wasiokuwa na ajira mkoani Kigoma.

"Lengo ni kuleta matokeo chanya kwa jamii kupitia kujengea uwezo kwa vijana katika sekta ya biashara, sana, ubunifu na utalii na mambo yote yanayohusiana na biashara ikiwemo kufawafanyia mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali na kuboresha biashara zao ili kuhakikisha wanakua kibiashara" alisema Mtiti.

Alisema, kwa upande wa utalii vijana wa Mkoa wa Kigoma wanayo fulsa ya kutengeneza ajira  kwa kuwa Mkoa wa Kigoma unahifadhi za Taifa za Gombe na Milima mahale pamoja na vivutio vingine vilivyopo katika Mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments