WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA VYUO VILIVYOPO MKOANI KIGOMA KUWAPATIA ELIMU VIJANA WAO

 

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa kigoma Deogratius Sangu (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa  Muwekezaji wa Chuo cha Uangazaji Ujiji (UBA) Baruan Muhuza kuhusu chumba kitakachotumika kwaajili ya mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi wa utangazaji. (Picha na Editha Karlo)


Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa kigoma Deogratius Sangu  akikagua studio ya Radio itakayotumiwa na wanafunzi wa utangazaji kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo. (Picha na Editha Karlo)

Muwekezaji wa Chuo cha Uangazaji Ujiji (UBA) Baruan Muhuza (Wa kwanza kushoto) akimueleza Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa kigoma Deogratius Sangu namna studio ya TV itakavyotumika kwaajili ya mafunzo kwa vitendo. (Picha na Editha Karlo)

Muwekezaji wa Chuo cha Uangazaji Ujiji (UBA) Baruan Muhuza akisoma risala yake kwa mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Deogratius Sangu (Hayupo Pichani)

Baadhi ya viongozi wa Dini na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi wa Chuo cha Uangazaji Ujiji (Ujiji Broadcasting Academy - UBA). (Picha na Editha Karlo)


Na Editha Karo,Kigoma

WAZAZI na walezi wametakiwa kutumia fursa ziliyopo katika Mkoa wa Kigoma kwa kutumia vyuo vilivyopo mkoani humo kuwapeleka vijana wao kupata elimu na taaluma mbalimbali zinazotolewa na vyuo hivyo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Chuo cha Utangazaji cha Ujiji (Ujiji Broadcasting Academy - UBA) Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kwa kuwakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa anayeshughulikia Uwekezaji na Biashara Deogratius Manumbu Sangu amesema fulsa kama hizi zinakuja kuufungua zaidi mkoa wa Kigoma na kuondoa usumbufu kwa wazazi kuepeleka watoto wao mikoa ya mbali kufuata vyuo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Sangu ameupongeza uongozi wa chuo cha UBA pamoja na bodi yake kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa chuoni hapo na kuleta chuo hicho mkoani hapa kwa wakati sahihi.

“Hiki ni chuo cha kwanza cha utangazaji katika Mkoa wetu na ni chuo cha kisasa naamini wanafunzi watakaosoma hapa watakuwa waandishi mahiri katika sekta ya uandishi wa habari hivyo nikupongeze muwekezaji wa chuo hiki na bodi kwa ujumla” amesema.

Andengenye amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu imeweka mazingira bora kwa wawekezaji katika nyanja zote hivyo serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji zaidi kuja kuwekeza mkoani kigoma.

Ameongeza kuwa, kupitia chuo hiki mkoa wa Kigoma unakwenda kuzalisha waandishi wa habari na watangazaji mahili ambao watasaidia kuutangaza mkoa wa kigoma kimaendeleo na kuibua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii ya watu wa Kigoma na taifa kwa ujumla ambapo serikali itazifanyia kazi.

“Nimefurahishwa na uwekezaji huu mkubwa wa elimu ndani ya Mkoa wetu ufunguzi wa chuo hiki utafungua fursa mpya ndani ya Mkoa wetu,muda wowote mkihitaji jambo lolote toka serikalini, ushauri karibuni milango ya ofisi yangu ipo wazi”alisema

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa Samson Shija amesema kuwa sekta habari na mawasilino ni sekta muhimu kwani imekuwa kama daraja la kuunganisha wananchi na serikali huku akiwaomba wadau na wananchi kukitumia chuo hicho ili kupata vijana wenye taaluma ya utangazaji kwa weledi.

“Sisi kama Ofisi ya Elimu ya mkoa tutatoa ushirikiano kwa kila kitu katika chuo hiki mana chuo kimesajiliwa na NACTE hivyo kinatambulika serikalini, na niwatoe hofu wazazi na walezi msihofu kuleta watoto wenu” amesema.

Nae Muwekezaji wa chuo cha UBA ambaye ndie Mkurugenzi mtendaji wa chuo hicho Baruan Muhuza mtangazaji wa kituo cha azam TV sambamba na kumiliki chuo hicho kwa 100% amesema alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwekeza kituo cha utangazaji mkoani Kigoma na hatimaye ametimiza ndoto hiyo.

“Ndoto yangu imekuwa kweli, na zaidi ya shilingili milioni 204 zimetumika katika uwekezaji wa chuo hiki ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vipya vya kisasa kwa msukumo wa elimu kwa vitendo.

“Ninawaalika watu wote toka ndani na nje ya Mkoa wa Kigoma na hata nchi za jirani  waje kwani chuo kina ithibati ya serikali, hivyo chuo hiki ni chenu tukitumie ili kupate watangazaji mahari kama mimi na wengine waliojipatia sifa ya kuwa watangazaji bora na waandishi mahari nchini” amesema Baruan

 

Post a Comment

0 Comments