WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZA TAIFA ZISIAJIRI WATU KUTOKA MOJA KWA MOJA VYUONI

Na, Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali za Taifa (Muhimbili, MOI, JKCI na Mloganzira) wasiajiri Madaktari mojo kwa moja kutoka vyuoni bali wawachukue walio Mikoani ambao wamekuwa na uzoefu wa muda mrefu.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo wakati akifungua Kongamano la 28 na Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji nchini Tanzania  unaofanyika Jijini Dodoma kwa siku Tatu wenye lengo la kujadiliana namna gani wanaweza kuboresha huduma za Ubingwa Bobezi nchini. 

Aidha, Waziri Ummy anaelezea dhamira ya Serikali kuanza mchakato wa kuwasambaza upya Madaktari Bingwa nchini ili kutatua changamoto ya uhaba wa madaktari hao katika maeneo yenye uhitaji mkubwa Mikoani.

Kauli mbiu “KUJENGA MFUMO WA UTOAJI HUDUMA ZA UPASUAJI MADHUBUTI, UNAOFIKIKA NA WENYE CHARAMA NAFUU TANZANIA”

Post a Comment

0 Comments