UTPC: USALAMA WA MWANDISHI KAZINI UZINGATIWE, WAPO HATARINI.

Na Diana Rubanguka, Kigoma.
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari   nchini-UTPC Kenneth Simbaya amewataka waandishi wa habari kutosita kutoa taarifa katika Klabu za waandishi wa habari zilizopo mikoani mwao wanapofanyiwa vitendo vya udharirishaji au kutishiwa usalama wao na wadau. 

Kenny Ameyasema hayo wakati akiongea na uongozi na wanachama wa chama cha waandishi habari mkoa wa kigoma (KGPC) ikiwa ni ziara yake maalumu kujitambulisha kwa wanachama lakini pia  kueleza namna ya ufanisi katika mpango wa Move From Good to Great unaolenga mabadiliko chanya ya press clubs nchini

Amesema zipo taarifa za wandishi wengi kufanyiwa madhira na wadau ikiwemo kushushwa njiani katika ziara, vitisho ubaguzi na unyanyapaa  mambo ambayo yanakwamisha ufanisi wa mwandishi kuripoti habari kwa maslahi ya umma

"Tunapaswa kufanya kazi kwa uhuru na katika mazingira salama, ikiwa umenyanyaswa fika press club yako mueleze mratibu atatolea taarifa madhira hayo kwa UTPC na UTPC inajua cha kufanya" alisisitiza Mkurugenzi UTPC.

Pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kukutana na wanachama wa kigoma press club kusisitiza umuhimu wa viongozi na wanachama katika press zote nchini kushirikiana, kudumisha mambo mazuri yaliyofanywa nakuwa na mipango thabiti kufanya mengine bora  zaidi na kuepuka migogoro isiyo na tija kwa ustawi wa wanachama.

Post a Comment

0 Comments