UTPC YALENGA KUBORESHA UTARATIBU KWA WANACHAMA KUJIFUNZA KUPITIA KLABU ZINGINE

Na Diana Rubanguka, Kigoma
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari   nchini-UTPC Kenneth Simbaya amesema UTPC inalenga kuboresha utaratibu wa viongozi na wanachama kutembelea klabu zingine kujifunza kulingana na mapungufu na makosa ili klabu zote ziweze kufikia lengo la kutoka pazuri kwenda pazuri zaidi(from Good to Great)
 
Simbaya ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika ofisi ya waandishi wa habari Mkoani Kigoma yenye lengo la kujitambulisha ambapo amesema miongoni mwa mambo ambayo yanahamasishwa kwa sasa ni kuweka utaratibu wa kutembelea klabu zingine kujifunza na kuleta mabadiliko ya kimazingira katika klabu.
 
“Nimetembelea klabu nyingi hapa nchini lakini klabu hii ya Kigoma kuna vitu vya kujifunza na  inaweza kuwa mfano mzuri kwa klabu zingine kujifunza na kujikosoa kulingana na mapungufu na makosa na iwe sababu ya kuzitoa klabu zao kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema.
 
Simbaya amesema wafadhili wamekuwa hawaoni maendeleo ya klabu zetu na hilo linatokana na wao kutotembelea klabu zingine ambazo ni mfano wa kuigwa na linatakiwa kutiliwa mkazo kwa kutangaza yale mazuri yaliyopo kwenye klabu zetu.
 
Sambamba na hilo amewasisitiza wanachama siku zote kuishi na kuitambua Dira na dhamira (Vission and Mission)  ya klabu kwa kuhakikisha wanazitumia popote pale hata wakati wa kijitambulisha ili kila mtu  aitambue klabu.

Nae Deogratius Nsokolo ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Kigoma na Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini UTPC amesema nidhamu katika utendaji kazi ni nguzo muhimu ya kutoka pazuri kwenda pazuri zaidi (Good to Great) hivyo nidhamu inahitajika ili kutambua tulipo na ni nini mfadhili anataka katika ulimwengu wa ufadhili.
 
"Chanzo cha migogoro katika Press Club zetu ni kutokuwa na nidhamu ya mtu mmoja mmoja na nidamu katika rasilimali za Klubu zetu, tuwe na akili za kufikiri, uongozi ufate misingi yake, kwa kuwa kosa la Press Club moja linaweza kuleta madhara kwa klabu zote nchni" amesema.
 
Kwa upande wake Afisa program na mafunzo wa UTPC Victor Maleko amesema bado kuna chngamoto ya waandishi kukutana na madhira wakati wa kazi na kuchukulia kama jambo la kawaida hivyo ametoa wito kwa waandishi kutolea taarifa matukio hayo.

Post a Comment

0 Comments