KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ARIDHISHWA NA MIRADI YOTE WILAYANI KIBONDO

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdallah Kaim ameridhishwa na utekelezaji Miradi 6 iliyotembelewa na mwenge huo katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma na kukubali kuizindua pamoja na kuweka Mawe ya Msingi. 

Pamoja na maelekezo Mengine, Kaimu amesema utekelezaji wa miradi mingi hususani ile ya Huduma za Jamii, wilaya imefanya vizuri kwani imezingatia viwango na ubora unaotakiwa na Serikali.

Akiwa katika mradi mkubwa wa maji mjini Kibondo, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge amesema mradi huo utakapokamilika utatimiza dhamira ya Rais Samia ya kumtua mama ndoo kichwani. 

Aidha Kaim amepongeza kazi nzuri inayofanywa na TARURA kwa kuendelea kuunganisha maeneo mbalimbali ya mkoa kupitia ujenzi wa madaraja  bora na yenye gharama nafuu kwa kutumia mawe. 

"Naelekeza maeneo yote tuliyobaini dosari mkazirekebishe mara moja na kazi hizo zifanyike ndani ya muda elekezwa" amesisitiza Kaim. 

Pia ameitaka jamii kuendelea kutunza Mazingira kwa kupanda miti na  kuepuka kuharibu vyanzo vya Maji.

Jumla ya miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bil 2 imetembelewa, kukaguliwa pamoja na kuwekewa mawe ya msingi wilayani Kibondo.

Post a Comment

0 Comments