MASHIRIKA KIGOMA YASHAURIWA KUTENGA BAJETI YA MAWASILIANO NA HABARI

Na Josephine Kiravu, Kigoma
Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Kigoma yametakiwa kuona namna ya kutenga bajeti kwa ajili ya wanahabari katika utekelezaji wa miradi yao ili kuwawezesha kufika maeneo ya vijijini ambayo ni changamoto kwao kufika kutokana na ukosefu wa fedha.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa klabu ya waandishi wa habari Kigoma (KGPC) Mwajabu Hoza wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Kigoma uliofanyika hivi karibuni.

Amesema baadhi ya viongozi wa mashirika hayo wamekuwa hawatengi bajeti kwa ajili ya wanahabari ambayo itawawezesha kufika maeneo ya vijijini na kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma.

Lakini pia changamoto ya baadhi ya mashirika kutotoa ushirikiano kwa madai ya sio wasemaji imekuwa kikwazo cha wanahabari kshindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

 ukamilisha majukumu hawathamini kile kinachofanywa na wanahabari kwa kuwazuia kuchukua taarifa wakati mwingi kuwanganya vifaa vya kazi ili tu wanahabari wasitekeleze majukumu yao.

Nao baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mratibu wa ulinzi wa mtoto kutoka Shirika la Save the Children Herbert Nkoko amewashauri wanahabari kuandaa maandiko na kuyapeleka kwenye mashirika ili iwe rahisi kupata ushirikiano huku akiahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wanahabari.

Post a Comment

0 Comments