MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAOMBWA KUANGALIA NAMNA YA KUSAIDIA WAKIMBIZI

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Serikali ya Tanzania imeomba mashirika ya Umoja wa matiafa yanayotoa huduma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu kuona namna ya kusaidia upatikanaji wa huduma muhimu kwa wakimbizi kwani huenda baadhi ya huduma muhimu ikiwemo chakula na huduma za afya  zikasitishwa kutokana na kupunguzwa kwa utoaji wa huduma kwa asilimia 30 kutoka kwa mashirika hayo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wakimbizi kutoka nchini Tanzania Sudi Mwakibase wakati alipotembelea kambi ya wakimbizi Nyarugusu akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani nchini Burundi.

Amesema kutokana na hali hiyo Tanzania inalazimika kuwarudisha wakimbizi  waishio katika kambi hiyo nchini kwao ili kuwaepusha na uhaba wa huduma muhimu ikiwemo chakula na afya.

Awali akitoa taarifa mbele ya ujumbe huo kutoka Burundi na Tanzania Kaimu Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu Hamphey Mrema amesema idadi ya wakimbizi wanaojiandikisha kurudi nchini kwao ni ndogo na hivyo kuathiri utoaji wa huduma kwa wakimbizi hao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani kutoka nchini Burundi amewahimiza warudi kurundi nchini kwao kwani nchi hiyo ina amani  huku akiomba mashirika ya umoja wa mataifa kutofunga utoaji wa huduma muhimu kwa wakimbizi katika kambi hiyo wakati serikali ikiendelea kutafuta namna ya kurudisha nyumbani.

Post a Comment

0 Comments