MIRADI 8 YENYE THAMANI YA BILIONI 1.5 YAKUBALIWA NA MWENGE WA UHURU 2023 WILAYANI KASULU

Na. Editha Karlo, Kasulu
MWENGE wa uhuru Kitaifa 2023 umeridhia miradi yote nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu yenye jumla ya shilingi bilioni 1.5.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023 Abdallah Shaibu Kaim amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo mwenge huo umepitia.

Kiongozi huyo amewataka watumishi wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili miradi ikamilike kwa wakati na wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Naye Mkuu Wilaya ya Kasulu kanali Izack Mwakisu amesema kuwa maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kama Wilaya wameyapokea na watayafanyia kazi.

“Nitasimamia maelekezo yote yaliyotolewa nitahakikisha ninayasimamia ili yafanyiwe kazi kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Kasulu na Taifa kwa ujumla”Amesema

Miradi iliyopitiwa na mwenge wa uhuru Kitaifa 2023 ni mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi moja ya waalimu, Kikundi cha waendesha bodaboda, kitalu cha kudumu cha kuotesha miti, mradi wa maji, mradi wa ujenzi vyumba vinne vya watumishi hospital ya halmashauri ya Wilaya.

Miradi mingine ambayo mwenge wa uhuru Kitaifa 2023 umeipitia ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami (0.5km) hospital ya Wilaya, mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na mradi wa mapambano dhidi ya UKIMWI pamoja na dawa za kulevya malaria na Lishe.

Post a Comment

0 Comments