MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA TSH. BIL. 18.3 KIGOMA

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake  mkoani Kigoma Agosti 16, 2023 ukitokea mkoani Kagera ambapo utatembelea, kukagua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi yenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Bil. 18.3 katika Halmashauri nane za Mkoa. 

Awali akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema miradi 21 itazinduliwa, mitatu kufunguliwa, 19 kuwekewa mawe ya Msingi pamoja na kutembelea mingine 21 huku miwili ikiwa ni ugawaji vyombo vya usafiri pamoja na vyakula kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI. 

Amesema miradi hiyo itazihusu Sekta za Afya, Huduma za Jamii, Kilimo, Ujenzi wa majengo na Barabara, Uhifadhi wa Mazingira pamoja na uwezeshaji kiuchumi kwa vikundi vya vijana, wanawake na watoto. 

Andengenye ameendelea kusisitiza kuwa, Mwenge wa Uhuru ni kichocheo  kwa Maendeleo na ni nguzo muhimu katika kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo ya watanzania kwa kudumisha uwazi, haki, umoja na mshikamano. 

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewasisitiza watendaji Serikalini kuendelea kusimamia kazi mbalimbali za miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali wakitanguliza uzalendo kwa manufaa ya wakazi wa Kigoma na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments