RC KIGOMA: KUKAMILIKA KWA RELI YA SGR FURSA KWA WAFANYABIASHARA MKOANI KIGOMA


Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kukamilika kwa ujenzi wa Reli ya SGR kutatoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kusafirisha bidhaa zao kwa muda mfupi na gharama nafuu hali itakayowaletea tija kiuchumi.

Andengenye ametoa kauli hiyo mara baada ya kukutana na Ujumbe kutoka Shirika  la Reli Tanzania (TRC) kwa lengo la kupokea Taarifa ya Maandalizi ya uwekwaji wa Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR)Km 506 kutoka Tabora hadi Kigoma.

Aidha mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa mradi huo utaongeza fursa za ajira pamoja na kupanua mzunguuko wa biashara mkoani Kigoma.

Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Albert Msovela amesisitiza kuwa, utoaji wa ajira zisizohitaji utaalam wakati wa utekelezaji mradi huo, utoe kipaumbele kwa wakazi wenyeji ili waweze kunufaika kiuchumi na kuziona faida za mradi kutekelezwa  katika maeneo yao.

Pia Msovela ametoa wito kwa wakazi mkoani Kigoma na nchi jirani kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazojitokeza wakati na baada ya ujenzi wa mradi huo.

Post a Comment

0 Comments