SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI WILAYANI KASULU KUNUFAIKA NA MFUKO WA JIMBO

Na Mwandishi wetu, Kasulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini kupitia Mfuko wa jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma amekabidhi madawati 722 kwa halmashauri ya Kasulu Mji ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini kwa mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.

Akikabidhi madawati hayo Mbunge wa jimbo hilo Prof. Joyce Ndalichako amefafanua kuwa madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 59 ambayo yatasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia huku akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha njia katika sekta ya Elimu.

Prof. Ndalichako amewasisitiza walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo ikiwa ni pamoja na kuonyesha nidhamu nzuri shuleni  pia amesisitiza kuendelea kutumia fedha ya jimbo kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu amemshukuru mbunge huyo kwa msaada huo wa madawati  na kueleza kuwa uwepo wake kwenye jimbo hilo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo na kuifanya wilaya hiyo kupiga hatua.

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa halmashauri ya Kasulu Mji Bw. Noel Hanura  ambaye ni diwani wa kata ya Heru Juu amemshukuru Prof. Ndalichako kwa kuwa mbunge Kiongozi ambaye pamoja na majukumu makubwa ya serikali aliyonayo amekuwa na utamaduni mzuri wa kukutana na wananchi na kutatua kero zao.

Aidha  Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kasulu Bw. Dollar Kusenge amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya Madawati ambapo hapo awali  halmashauri  ilikuwa na upungufu wa madawati 22,500 na pia ameendelea kumshukutu Rais  samia kwani ameboresha mazingira latika nyanja za elimu, afya  na mazingira  kwa kuleta watumishi wa kutosha.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari bogwe Bw. David Kindanda  kwa niaba ya walimu wakuu wote amesema "Naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji kwani madawati tuliyopewa leo yatasaidia kupandisha kiwango cha taaluma na kupunguza utoro".

Post a Comment

0 Comments