WATENDAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA WAZAZI WANAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO YA POLIO

Na Mwandishi Wetu, Kasulu Kigoma
Watendaji wa Kata na Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha wananchi wanawapeleka watoto wenye umri wa chini ya miaka nane kwenda kupata chanjo ya ugonjwa wa Polio. 

Hayo yamebainishwa leo wilayani humo na  Afisa  Usafi na Udhibiti wa Taka wa halmashauri hiyo, Ndelekwa Vanica aliyemwakilisha Mkurugenzi, Joseph Kashushura katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Polio.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeona umuhimu wa kuendesha zoezi hilo katika mikoa sita ya Kigoma, Mbeya, Rukwa, Katavi, Songwe na Kagera litakalochukua muda wa siku nne.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kampeni Ngazi ya Mkoa, Dr Godfrey Smart amesema kuwa zoezi hilo limefanyika katika mikoa hiyo baada ya mkoa jirani wa Katavi  mtoto kubainika kuumwa ugonjwa huo. 

Pia amebainisha kuwa  mkoa wa Kigoma umepanga kuwachanja watoto wapatao  884,000 na chanjo hiyo ni salama  kwa kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Wizara ya Afya. 

Post a Comment

0 Comments