RC ANDENGENYE AAGWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI







Na Mwandishi Wetu, Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, ameagwa rasmi katika Utumishi wa Jeshi hilo.

Hafla ya kumuaga imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Kilichopo Chogo Wilaya ya  Handeni Mkoani  Tanga.

Andengenye alistaaafu rasmi wadhifa huo tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Julai 3, 2020 ambapo alitumikia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzia Mwaka 2016 hadi 202O.

Kabla ya kutumikia Jeshi hilo,  Andengenye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,  Arusha na Kamishna wa Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments